Loading...

19 wameuawa kwenye Shambulio la kigaidi katika tamasha la muziki nchini Uingereza

Watu 19 wameuawa na wengine 50 kujeruhiwa baada ya bomu kulipua ukumbi wa tamasha la muziki, katika mji wa Manchester, Uingereza.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ametaja tukio hili kama kitendo cha ugaidi.

Iwapo shambulio hilo litathibitishwa kuwa ni la kigaidi, linatajwa kuwa ni baya zaidi kuwahi kuikumba Uinereza.

Shambulio kubwa zaidi lilitokea Julai 2005 ambapo watu zaidi ya 50 walipoteza maisha baada ya kutokea mlipuko, jijini London.

Katika tukio la jana, mashuhuda wanasema shambulio hilo lilitokea mara tu baada ya mwanamuziki wa Marekani Ariana Grande kumaliza kuwatumbuiza mashabiki wake.

Mashudhuda wa tukio hilo wamesema waliona misumari iliyotapakaa sakafuni na harufu ya mabomu.

Eneo kulikotokea mulipuko huo limezingirwa na polisi waliojihami wanaendelea kushika doria.

Wakati huo huo Waziri Mkuu Theresa May anatarajiwa kuongoza kikao cha dharura cha kamati ya usalama baadaye leo.
19 wameuawa kwenye Shambulio la kigaidi katika tamasha la muziki nchini Uingereza 19 wameuawa kwenye Shambulio la kigaidi katika tamasha la muziki nchini Uingereza Reviewed by Zero Degree on 5/23/2017 11:12:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.