Loading...

Abramovic kumwagia Conte mamilioni kwa ajili ya usajili wa nyota wanne

Mimiliki wa The Blues, Roman Abramovic inaonekana yuko tayari kumpa Conte kiasi cha paundi milioni miambili [£200M] kama bajeti kwa ajiri ya kukamilisha usajili wa majira ya joto.

Kama ambavyo Chelsea wanajiandaa kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa, Conte bila shaka lazami atakuwa katika mipango ya kuimarisha kikosi chake.

Na taarifa za leo zinasema kwamba Abramovich anamuunga mkono muitaliano huyo kwa kujaza mifuko yake na pesa za kutosha kwa ajili ya shughuli ya usajili wa wachezaji wapya, ambapo unaweza kuona nyota Morata wanatua Stamford Bridge bila matatizo.

Kwa mujibu wa taarifa, Roman Abramovich yuko tayari kuingia na nguvu zote katika soko la usajili ikiwa ni katika harakati za kusaka wachezaji wanne wenye uwezo mkubwa msimu huu.

Antonio Conte daima aliweka wazi msimu huu kwamba anapanga kufanya mapinduzi katika Ligi ya Mabingwa msimu ujao kama walivyofanya katika ngazi ya ndani katika kampeni yake ya kwanza ya kusaka taji la Ligi Kuu, hata hivyo, wakosoaji wanasema kwamba ili afanikiwe kufanya hivyo itamlazimu kutumia pesa nyingi.

Inawezekana kabisa ripoti hii ikawa ni ya kweli, bila shaka Abramovich atampa 'sapoti' Conte kwa uhamisho wowote atakaotaka kufanya, historia inaonyesha kuwa mmiliki wa Chelsea amekua akitoa fedha kwa kila uhamisho ambao 'The Blues' wamekuwa wakifanya.

Na kwa kiasi kikubwa cha fedha ambachi Chelsea watapokea kwa kushinda Ligi Kuu ya Uingereza, hakika lazima kutakuwa na ongezeko 
kidogo katika matumizi  ya fedha kwa kuzisambaza duniani kwenye kinyang'anyiro cha usajili.
Abramovic kumwagia Conte mamilioni kwa ajili ya usajili wa nyota wanne Abramovic kumwagia Conte mamilioni kwa ajili ya usajili wa nyota wanne Reviewed by Zero Degree on 5/15/2017 05:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.