Loading...

Alichosema Mourinho kuelekea mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Europa dhidi ya Celta Vigo leo

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amesema kwamba haamini kwamba anacheza kamari kwa kuangazia zaidi ubingwa wa ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League.

Meneja huyo, ambaye ameamua kuangazia ligi hiyo badala ya kumaliza katika nafasi nne za kwanza Ligi Kuu ya Uingereza, anasema uamuzi wake ni wa busara.

United wanaongoza 1-0 dhidi ya Celta Vigo goli la nusufainali kwanza ambapo wanaelekea kukutana kwa ajili ya mechi ya marudiano leo Alhamisi usiku kwenye uwanja wa Old Trafford.

Mourinho amesema kuwepo kwa mechi nyingi ambazo klabu yake inahitajika kucheza kumemlazimu kuamua ataangazia wapi.

"Kucheza mechi kumi na saba katika wiki saba haiwezekani. Si kamari, ni matokeo tu ya hali ilivyo," alisema.

"Ulikua uamuzi rahisi sana kuufanya, uamuzi wa busara."

Mabingwa wa Europa League huhakikishiwa nafasi katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, sawa na klabu zinazomaliza naafsi nne za kwanza Ligi ya Premia.

Manchester United walishuka hadi nafasi ya sita Jumatano baada ya Arsenal kuwalaza Southampton 2-0 Jumatano.

Arsenal waliwalaza United Jumapili katika mechi ambayo Mourinho aliwapumzisha wachezaji wengi wake nyota kwa ajili ya mechi ya Alhamisi.

Mourinho anaamini kwamba kushinda Europa League ndio njia nzuri zaidi iliyosalia ya kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Amesema hatakuwa na majuto kamwe iwapo watashindwa kutwaa ubingwa. "Hebu tusubiri tuone kama tutaweza," alisema.

"Haijalishi nini kitatokea. Hakuna majuto, tutajitolea kadiri ya uwezo wetu, mimi na wachezaji."

Mshambuliaji wa United Wayne Rooney anaunga mkono msimamo wa Mourinho.

"Kusema kweli, ni vigumu kufuzu kwa kupitia ligi. Tunaweza tukaangazia kushinda kikombe."
Alichosema Mourinho kuelekea mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Europa dhidi ya Celta Vigo leo Alichosema Mourinho kuelekea mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Europa dhidi ya Celta Vigo leo Reviewed by Zero Degree on 5/11/2017 04:43:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.