Loading...

Antony Joshua kuingia ulingoni tena mwisho wa mwaka

Bingwa wa Dunia uzito wa juu, Anthony Joshua, huenda akaingia ulingoni mwezi wa Novemba, tayari kutetea ubingwa wake wa Dunia. Katika kuelekea pambano hilo mpaka sasa, tayari kumbi za mpambano huo zimeanza kupendekezwa.

Joshua ataingia ulingoni kutetea taji lake katika kipindi cha majira ya baridi.

“Kuna uwezekano mkubwa” wa kupambana tena mwezi November mwaka huu,” Alisema promoter wake, Eddie Hearn, kumbi zilizopendekezwa mpaka sasa ni za Wales, America, China pamoja na Dubai, hii ikiwa ni kwa ajili ya kulitetea taji lake la Dunia.

Bingwa huyo wa WBA na IBF uzito wa juu, ata ufahamisha ulimwengu kama atapigana na Klitschko katika mchezo wa marudiano, baada ya kumshinda katika raundi ya 11 katika uwanja wa Wembley mwezi uliopita.
Antony Joshua kuingia ulingoni tena mwisho wa mwaka Antony Joshua kuingia ulingoni tena mwisho wa mwaka Reviewed by Zero Degree on 5/16/2017 03:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.