Loading...

Ben Pol alivyozua gumzo kwa Picha ya nusu utupu

Msanii wa Bongo Fleva, Ben Pol amejikuta akizua minong’ono kwa mashabiki wake na Watanzania kiujumla baada ya kuposti picha akiwa nusu utupu kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Picha aliyopost Ben Pol
Kwenye picha hiyo Ben Pol hakuweka maneno yoyote yale lakini alionekana amefungwa na kamba kama mtu aliyetekwa.

Picha hiyo iliyowekwa jana usiku mpaka sasa ina maelfu ya likes na Maoni kibao ya mashabiki wake wengi wakionekana kukerwa na kitendo hicho.

Ikumbukwe mwaka jana Wema Sepetu alifuta picha zake zote instagram na aliporejea katika mtandao huo January 28 mwaka huu, February 3 alitangaza ujio wa app yake. Mwanamuziki Mwasiti naye aliwahi kufuta picha zote na aliporejea December 13 mwaka jana alitangaza ujio wa wimbo wake mpya ‘Kaa Nao’

Ben Pol nae amefanya kama wao, bila shaka kuna kitu kipya kina kuja kutoka kwake, ila picha aliyoweka kabla hata hatujajua nini kinafuata imezua gumzo na majadala mzito huko wengine wakikosoa vikali picha hiyo. Itazame hapa chini.


Hapo chini ni maoni ya baadhi ya mashabiki walioiona picha hiyo:




Ben Pol alivyozua gumzo kwa Picha ya nusu utupu Ben Pol alivyozua gumzo kwa Picha ya nusu utupu Reviewed by Zero Degree on 5/19/2017 07:56:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.