Loading...

BreakingNews: Mmiliki wa Shule ya Lucky Vicent Arusha afikishwa mahakamani kwa makosa matano

Mmiliki wa shule ya Lucky Vicent Arusha, Innocent Moshi na Makamu Mkuu wa shule Longino Vicent Nkana wamefikishwa Mahakamani na kusomewa makosa matano.

Mwendesha mashtaka wa Serikali Rose Sule amesema mnamo May 6 Mmiliki huyo wa shule aliruhusu Dereva kuendesha gari la abiria bila kuwa na leseni ya usafirishaji, kutumia gari bila kuwa na BIMA pamoja na kushindwa kuingia mkataba na Mwajiriwa.

Makosa mengine ni kuzidisha abiria 13 kwenye gari pamoja kaimu mkuu wa chuo kuratibu safari pamoja na kuruhusu gari kuzidisha abiria.

Watuhumiwa wote wameachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuwa na watu wawili kwa bondi ya milioni 15 kila mmoja na huku washtakiwa kutoruhusiwa kuondoka ndani ya mkoa ikiwa ni pamoja na kuwasilisha hati zao zakusafiria.

Hakimu wa Mahakama ya hakimu mkazi aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Desdery Kamugisha ameahirisha kesi hiyo mpaka 8 mwezi wa 6 kutokana na upelelezi kutokamilika.
BreakingNews: Mmiliki wa Shule ya Lucky Vicent Arusha afikishwa mahakamani kwa makosa matano BreakingNews: Mmiliki wa Shule ya Lucky Vicent Arusha afikishwa mahakamani kwa makosa matano Reviewed by Zero Degree on 5/12/2017 04:38:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.