Loading...

Chelsea, Manchester City zaingia vitani kusaka saini ya kinda huyu

Kinda wa Juventus, Kingsley Coman ameeleza kwamba yuko kwenye mikakati ya kuondoka katika klabu ya Bayern Munich ambako yupo kwa mkopo.

Winga huyo amecheza mechi 19 za Bundesliga akiwa na Bayern Munich ambao ndi mabingwa wa Ligi hiyo kwa msimu ulioisha, na nyingi kati ya mechi hizo alitokea benchi.

Vilabu vingi vikubwa vinavyoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza vimeripotiwa kumhitaji Coman kufuatia ripoti inayodai kinda huyo hana raha kabisa kukosa nafasi ya kushiriki na kikosi cha kwanza mara kwa mara.

Nyota huyo mwenye miaka 20 amewaka wazi kuwa mpango wake wa kuondoka Bayern umetawala zaidi kichwani mwake.

Imeripotiwa kwamba, Chelsea na Manchester City wameagiza watu wanajeshi wao kuchunguza hatua zote za kinda huyo, lakini hakuna klabu hata moja kati ya hizo iliyokwisha peleka ofa mezani.


Coman alisema: “Ulikuwa ni mwaka mgumu sana kwangu mimi. Hadi nilifikiria kuhusu kuondoka Bayern.

“Ni vigumu sana kufanikiwa kupata nafasi ya kudumu katika timu na kupata nafasi ya kuanzia kikosi cha kwanza mara kwa mara pale kocha anapokua ameteua kikosi chake cha kwanza, hasa hapa Bayern kwa sababu ya ushindani mkubwa wa nafasi ya kucheza

“Lakini Bayern walinipa hisia kwamba wana mipango ya muda mrefu na mimi, ukijumuisha pia na msimu ujao. Waliniambia niendelee kufanya juhudi za kutosha na mwisho mambo yatakuwa mazuri.”
Chelsea, Manchester City zaingia vitani kusaka saini ya kinda huyu Chelsea, Manchester City zaingia vitani kusaka saini ya kinda huyu Reviewed by Zero Degree on 5/30/2017 11:09:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.