Loading...

Conte ameweka wazi mikakati yake ya usajili ujao baada ya msimu huu kuisha

Kocha wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte amekiri kwamba klabu yake inahitaji wachezaji wapya kwa ajili ya kuongeza nguvu zaidi katika msimu ujao.

Kama ambavyo Chelsea wanajiandaa kuingia katika Ligi ya Mabingwa msimu ujao, wanahitaji kurekebisha baadhi ya mapungufu yao, na Conte yuko tayari kuleta nguvu mpya Stamfrod Bridge.

'The Blues' itashiriki katika mashindano manne kwa msimu ujao, na Conte anatambua kwamba kikosi chake cha sasa bado kina udhaifu mkubwa wa kuweza kushindana katika mashindano yote manne na kumaliza katika nafasi nzuri.


Hata hivyo, tayari Conte ameonekana kufikiria mbele zaidi:

"Usisahau kwamba Tottenham walitolewa kwenye Ligi ya Mabingwa katika hatua ya makundi, na kisha wakatolewa nje katika raundi ya kwanza ya Europ (hatua ya mtoano), " alisema.

"Kama ukifikiria kiasi cha michezo yetu na michezo yao, kuna tofauti ya nini, ni kama mechi nane hivi....

"Lakini kama ukifikiria vikosi, ukija kwa idadi katika kila kikosi, unaweza kuona tofauti: timu moja iko tayari kucheza Ligi ya Mabingwa na wachezaji 25 au 26, na wengine ambao wako tayari kucheza Ligi Kuu, FA na Kombe la Ligi .


"Je, tunahitaji wachezaji zaidi? Hakika jibu lake ni Ndiyo." 


'The Blues' watacheza dhidi ya Middlesbrough usiku wa leo wakijua kwamba ushindi unawaweka juu zaidi na kuwapa uhakika wakuzidi kulinyemelea kombe la Ligi Kuu.

Mechi za Chelsea zilizobakia katika msimu wa Ligi Kuu na FA 2016/17 ni:

  • Chelsea Vs Middlesbrough (Nyumbani) - Jumatatu Mei 8
  • Chelsea Vs West Brom (Ugenini) - Ijumaa ya Mei 12
  • Chelsea Vs Watford (Ugenini) - Jumatatu ya Mei 15
  • Chelsea Vs Sunderland (Nyumbani) - Jumapili ya Mei 21
  • Chelsea Vs Arsenal Fainali ya kombe la FA (Wembley) - Jumamosi ya Mei 27
Conte ameweka wazi mikakati yake ya usajili ujao baada ya msimu huu kuisha Conte ameweka wazi mikakati yake ya usajili ujao baada ya msimu huu kuisha Reviewed by Zero Degree on 5/08/2017 07:13:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.