Loading...

Mtihani wa kwanza kwa Himid Mao nchini Denmark

Kiungo mkabaji wa Azam FC, Himid Mao, kesho Jumanne anatarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza wa majaribio akiwa na kikosi cha akiba cha timu ya Randers, inayoshiriki ligi kuu ya nchini Denmark.

Himid ambaye aliondoka nchini wiki iliyopita kwenda nchini humo ambapo muda mrefu alikuwa akitakiwa na timu ya Mamelods Sundowns ya Afrika kusini, amechagua kwenda Denmark kutokana na kuamini kwamba ndiyo sehemu sahihi kutimiza ndoto zake ambapo atafanya majaribio hayo kwa muda wa siku kumi.

Rasmus Bertelsen, ambaye ndiye 
Skauti mkuu wa kusaka vipaji wa timu hiyo alisema kuwa kiungo huyo atakuwepo katika mechi hiyo ya kikosi cha akiba cha timu hiyo kabla ya kuamua kumsajili.

“Himid lazima awe sehemu ya klabu yetu katika mechi ya wachezaji wa akiba dhidi ya AC Horsens ambayo itachezwa kesho Jumanne, naamini ataonyesha kile ambacho tunakitegemea kutokana na uwezo wake.

“Nadhani tunatarajia kumsajili katika timu yetu kwa sababu kabla ya kuja hapa, tulikuwa tunamfuatilia, ndiyo maana kwanza majaribio yake yalianzia katika timu ya vijana kabla ya kumpandisha ili acheze mchezo wa kesho,” alisema Bertelsen.
Mtihani wa kwanza kwa Himid Mao nchini Denmark Mtihani wa kwanza kwa Himid Mao nchini Denmark Reviewed by Zero Degree on 5/08/2017 07:31:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.