Loading...

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma kutua nchini kwa ajili ya ziara ya siku 3

RAIS wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, anatarajiwa kufanya ziara ya kitaifa ya siku tatu hapa nchini kuanzia Mei 10 hadi 12 mwaka huu.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushiriano wa Kimataifa, Dk. Agustine Mahiga akizungumza na waandishi wa habari.
Kiongozi huyo anakuja kutokana na mwaliko wa Rais John Magufuli kufuatia kukutana kwao mjini Addis Ababa Ethiopia kwenye mkutano wa 28 wa wakuu wa nchi na serikali wa umoja wa Afrika (AU).

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushiriano wa Kimataifa, Dk. Agustine Mahiga ambapo ziara hiyo itatoa fursa kwa viongozi kujadili masuala mbalimbali yanayohusu nchi hizo mbili ya kikanda na kimataifa na kuangalia namna ya ushirikiano katika maeneo ya uwekezaji na biashara katika kukuza na kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Zuma anatarajiwa pia kufungua rasmi jengo jipya la ubalozi wa Afrika Kusini nchini na kutembelea Taasisi ya Matibabu ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma kutua nchini kwa ajili ya ziara ya siku 3 Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma kutua nchini kwa ajili ya ziara ya siku 3 Reviewed by Zero Degree on 5/08/2017 07:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.