Loading...

Maradona amepata shavu jipya Uarabuni

Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Barcelona Muargentina, Diego Maradona ’56’ baada ya kibarua chake cha kuinoa klabu ya Al Wasl kuota nyasi, hatimaye amepata klabu ya kuitumikia.

Diego Maradona amepata shavu la kuinoa klabu ya Al-Fujairah FC, ya Uarabuni kama kocha mkuu hii ikiwa ni kazi yake ya kwanza kwa miaka mitano toka afukuzwe na klabu ya Al Wasl mnamo July 2012.

Klabu ya Al-Fujairah kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii waliweka picha ya Maradona na kuthibitisha usajili huo.

Diego Maradona kwenye dili hilo ataingiza kiasi cha Dola 800,000 za Kimarekani na ameahidiwa kuongezewa mkwanja endapo klabu hiyo itachukua kombe lolote kwa msimu huu.
Maradona amepata shavu jipya Uarabuni Maradona amepata shavu jipya Uarabuni Reviewed by Zero Degree on 5/08/2017 07:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.