82 kati ya zaidi ya wanafunzi 270 waliotekwa na Boko Haram mwaka 2014 waachiwa huru
Mmoja waliotekwa nyara akiongea baada ya kupatikana |
Kwa mujibu wa habari zilizothibitishwa na Ikulu ya Nigeria, wasichana hao wameachiwa huru wakiwa salama kufuatia majadiliano ya muda mrefu na ubadilishanaji washukiwa wa Boko Haram, waliokuwa wamezuiliwa na serikali ya nchi hiyo.
Wasichana waliotekwa nyara kutoka shule moja iliyopo katika Mji wa Chibok, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria mwaka 2014 |
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa BBC, Stephanie Hegarty kutoka Lagos, wasichana hao wote 82 kwa sasa wanalindwa na jeshi la Nigeria mahali salama, baada ya kutolewa kutoka mafichoni kwa barabara kutoka maeneo ya ndani kabisa vijijini, hadi katika Kambi ya Jeshi ya Banki, karibu na mpaka na Cameroon.
Mwandishi huyo anasema kuwa, familia nyingi huko Chibok zimefurahia taarifa hiyo ya hivi punde lakini wapiganaji hao wa Boko Haram, wangali wakiwazuilia zaidi ya wanafunzi 100.
Kabla ya hatua hii ya hivi punde ya kuwaachia wasichana hao, inakisiwa kuwa zaidi ya wasichana 195 wangali hawajulikani waliko.
Idadi ya washukiwa wa Boko Haram ambao wameachiwa huru na utawala wa Nigeria, bado haijajulikana.
82 kati ya zaidi ya wanafunzi 270 waliotekwa na Boko Haram mwaka 2014 waachiwa huru
Reviewed by Zero Degree
on
5/08/2017 07:57:00 PM
Rating: