Loading...

Orodha ya mabondia wa timu ya taifa iliyotolewa na BFT

Mabondia hao ishirini (20) kati yao wakiwemo wanaume kumi na watano (15) na wanawake watano (5). Uteuzi huo umefanywa na kamati ya ufundi ya BFT ikiwa chini ya Kocha David Yombayomba, kocha Mkuu wa timu ya ngome akishirikiana na makocha wa timu zote zilizoshiriki mashindano ya ngumi ya taifa yanayomalizika 30/04/2017 Kawe, jijini Dar es salaam.

Uteuzi huo umezingatia uwezo wa sasa wa kucheza mchezo wa ngumi, umri unaokubalika kwa mujibu wa sheria za chama cha ngumi cha dunia (AIBA) na tabia binafsi ndani na nje ya ulingo.

Majina ya mabondia na uzito wao ni kama ifuatavyo:-

Light Fly weight 49 Kgs
  • Herman Richard (Ngome)
Fly weight 52 Kgs
  • Ibrahim Aballah (Urafiki)
  • George Costantino (Ngome)
Bantam weight 56 Kgs
  • Ezra Paulo ( Ngome)
Light weight 60 Kgs
  • Ismail Galiatano (Ngome) King Lucas (Kigoma)
Light welter 64 Kgs

  • Mohamed Juma (Ngome)
  • kassim Seleman (Ngome)
Welter 69 Kgs
  • Said Ramadhan (JKT)
  • Haruna Hussein (JKT)
Middle weight 75 Kgs
  • Seleman Kidunda
Light heavy weight 81 Kgs
  • Yusuph Changarawe
Heavy Weight 91 Kgs
  • Haruna swanga (Ngome)
Super Heavy weight 91+
  • Mhina Morris (Ngome)
  • Alex Sitta (JKT)
Kwa upande wa wanawake waliochaguliwa ni Sara Andrew ( Ngome), Grace Joseph (JKT), Siwatu Eliuta (JKT), Sarafina James (JKT) na Aliskunda Jonas (Kigoma). 

Tarehe 8/5/2017 (leo) shirikisho litaanza hatua ya kuwaombea ruhusa kutoka kwa aajili ya kuanza mazoezi haraka iwezekanavyo ili kushiriki mashindano ya Ubingwa wa Afrika yatakayofanyika Congo Brazzaville 25/05-04/06/2017.

Pia baadhi yao watakwenda kushiriki mashindano ya Afrika mashariki yatakayofanyika Kampala Uganda mwishoni mwa mwezi huu.
Orodha ya mabondia wa timu ya taifa iliyotolewa na BFT Orodha ya mabondia wa timu ya taifa iliyotolewa na BFT Reviewed by Zero Degree on 5/08/2017 08:21:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.