Dikteta wa zamani wa nchi ya Panama, Manuel Noriega afariki dunia
Dikteta wa zamani wa Panama Manuel Noriega kwenye picha iliyopigwa mwaka 2011 |
Noriega alifanyiwa upasuaji hivi majuzi baada ya kuanza kuvuja damu kufuatia upasuaji kwenye ubongo wake.
Noriega awali alikuwa mshirika mkuu wa Marekani lakini aliondolewa madarakani kwa nguvu wanajeshi wa Marekani walipovamia nchi yake mwaka 1989.
Baadaye, alifungwa jela Marekani baada ya kupatikana na makosa ya ulanguzi wa madawa ya kulevya na utakatishaji wa pesa.
Alipatikana pia na makosa Ufaransa, na kisha Panama, ya mauaji, ufisadi na wizi wa mali ya umma.
Alikuwa ameachiliwa huru kutoka gerezani Januari kumruhusu kufanyiwa upasuaji kwenye ubongo wake.
Noriega awali alikuwa mshirika mkuu wa Marekani lakini aliondolewa madarakani kwa nguvu wanajeshi wa Marekani walipovamia nchi yake mwaka 1989.
Baadaye, alifungwa jela Marekani baada ya kupatikana na makosa ya ulanguzi wa madawa ya kulevya na utakatishaji wa pesa.
Alipatikana pia na makosa Ufaransa, na kisha Panama, ya mauaji, ufisadi na wizi wa mali ya umma.
Alikuwa ameachiliwa huru kutoka gerezani Januari kumruhusu kufanyiwa upasuaji kwenye ubongo wake.
Dikteta wa zamani wa nchi ya Panama, Manuel Noriega afariki dunia
Reviewed by Zero Degree
on
5/30/2017 09:07:00 AM
Rating: