Loading...

Everton kukipiga na nyota wa Tanzania mwezi Julai mwaka huu

Klabu ya Uingereza ya Everton itazuru nchini Tanzania kwa mechi za kirafiki kabla ya msimu wa 2017/18.

Kampuni ya Sportpesa baada ya kuweka mkataba wa kuidhamini klabu ya Everton kutoka Uingereza
Kulingana na tovuti rasmi ya klabu hiyo, ziara hiyo ambayo ni ya kusheherekea udhamini mpya wa klabu hiyo na Sportpesa itakuwa na mechi ya kirafiki kati ya klabu hiyo na nyota wa Tanzania katika uwanja Taifa wa Dar es salaam wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000 tarehe 13 Julai.

Everton itakuwa klabu ya kwanza ya ligi ya Uingereza kucheza katika taifa hilo la Afrika Mashariki, na itakabliana dhidi ya mshindi wa kombe hilo la Sportpesa.

Mchuano huo utashirikisha timu kutoka Tanzania na Kenya ambazo zitatoa timu nne kila moja wao.

Mapema mwezi huu Everton ilitangaza udhamini wa mamilioni ya pesa na Sportpesa ambapo jina la kampuni hiyo ya kamare litakuwa mbele ya tisheti za mabingwa hao wa Uingereza kwa miaka mitano.

Tangu kuanzishwa kwake nchini Kenya 2014 kampuni hiyo imedhamini vilabu vingi, kuwekeza mbali na kushiriki katika kamari.
Everton kukipiga na nyota wa Tanzania mwezi Julai mwaka huu Everton kukipiga na nyota wa Tanzania mwezi Julai mwaka huu Reviewed by Zero Degree on 5/26/2017 01:52:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.