Loading...

Fainali ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba dhidi ya Mbao FC kuchezwa Mei 28 mjini Dodoma

Hatimaye fainali ya Kombe la Shirikisho kati ya Mbao FC dhidi ya Simba itafanyika Mei 28 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas amethibitisha kwamba uwanja utakuwa ni Jamhuri.

"Kweli ni Jamhuri, awali ilikuwa ni droo lakini sasa moja kwa moja tumetangaza Jamhuri," alisema leo.

Awali, kupitia mitandao ya kijamii, Rais wa TFF, Jamal Malinzi alitangaza uwanja utakaochezewa mechi utapatikana kupitia droo.

Malinzi alisema droo itafanyika ndani ya siku chache zijazo jambo ambalo lilizua mjadala mkubwa kati yake na mashabiki ambao walioenkana kumshangaza.
Fainali ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba dhidi ya Mbao FC kuchezwa Mei 28 mjini Dodoma Fainali ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba dhidi ya Mbao FC kuchezwa Mei 28 mjini Dodoma Reviewed by Zero Degree on 5/02/2017 04:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.