Loading...

TFF imekanusha Taarifa inayosambaa mitandaoni kuhusu FIFA kutoa majibu ya rufaa ya Simba SC

Taarifa hiyo ilidai kuwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limeijibu barua ya rufaa ya Klabu ya Simba ambayo ilipeleka maombi ya kupinga Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) kuipa Kagera Sugar pointi tatu.

Katika barua hiyo ya majibu ya FIFA, shirikisho hilo imetupilia mbali maombi ya Simba kupinga uamuzi huo wa TFF kwa Simba, hivyo kwa maana hiyo, Yanga inaendelea kuwa bingwa kutoka na maamuzi hayo ambayo hayatabadili msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom 2016/17.

Hata hivyo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema kwamba hiyo taarifa sio ya kweli kwani wao hawajaipokea barua hiyo.

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas kwa njia ya simu [alipotafutwa na mtandao wa SalehJembe] amesema kwamba hakuna barua hiyo.

“Niko nje ya ofisi, lakini nimeulizia ofisini inaonekana hakuna barua kama hiyo iliyopokelewa,” alisema.

“Sijui labda tuendelee kusubiri, kama kuna kitu nitakujulisha ila hadi sasa hakuna barua.”

TFF imekanusha Taarifa inayosambaa mitandaoni kuhusu FIFA kutoa majibu ya rufaa ya Simba SC TFF imekanusha Taarifa inayosambaa mitandaoni kuhusu FIFA kutoa majibu ya rufaa ya Simba SC Reviewed by Zero Degree on 5/27/2017 07:04:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.