Loading...

FIFA imetuma salamu za pongezi kwa Yanga baada ya kunyakua ubingwa wa VPL

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania la Kimataifa (Fifa), Gianni Infantino
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania la Kimataifa (Fifa), Gianni Infantino, ametuma salamu za pongezi kwa timu ya Yanga baada ya kuwa mabingwa Ligi Kuu Bara msimu wa 2016/17.

Fifa imeipongeza Yanga baada ya kumaliza msimu ikiwa kileleni na pointi 68 ambazo ni sawa na za Simba, lakini Yanga imeweza kuwa bingwa kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa ambayo ni kumi.

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
Salamu za Fifa kwa Yanga zimewasilishwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi baada ya leo kuandika kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii wa Twitter.

Ujumbe wa Malinzi Twitter
Wakati Fifa inaipongeza Yanga kwa kutwaa ubingwa huo, watani zao wa jadi, Simba bado wanadai kupewa pointi zao tatu ambazo awali walipewa na Kamati ya Saa 72 kutokana na kumkatia rufaa beki wa Kagera Sugar, Mohammed Fakhi ambaye anadaiwa kucheza dhidi yao akiwa na kadi tatu za njano jambo ambalo ni kinyume na kanuni za Ligi Kuu Bara. Katika mchezo huo, Simba ilikubali kichapo cha mabao 2-1.

Baada ya Simba kupokwa pointi hizo na Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji, viongozi wa klabu hiyo wakaenda kukata rufaa Fifa ambapo mpaka shirikisho hilo linatuma pongezi zake kwa Yanga kuwa bingwa, bado Simba haikuwa imepewa majibu ya rufaa yao kama imeshinda au la.
FIFA imetuma salamu za pongezi kwa Yanga baada ya kunyakua ubingwa wa VPL FIFA imetuma salamu za pongezi kwa Yanga baada ya kunyakua ubingwa wa VPL Reviewed by Zero Degree on 5/24/2017 03:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.