Loading...

Huu ndio ujumbe alioutuma Nemanja Matic kwa kocha wa West Ham

Kiungo wa Chelsea, Nemanja Matic amemtumia meseji kocha wa West Ham United, Slaven Bilic kwamba atampeleka kula chakula cha usiku kama timu yake itaichapa Tottenham Hotspur na kuipa The Blues nafasi ya kubeba taji la Ligi Kuu England msimu huu kitu ambacho kimetimia kweli.

Spurs ilikuwa ikiitisha Chelsea kwenye mbio za ubingwa, lakini baada ya kipigo tu cha bao 1-0 kutoka kwa West Ham United Ijumaa iliyopita kilitoa fursa kwa Chelsea kukamatia ubingwa na kama itakuwa imeshinda kwenye mechi yao ya usiku wa jana Jumatatu dhidi ya Middlesbrough uwanjani Stamford Bridge, basi watakuwa wameweka mkono mmoja kwa taji hilo.

Chelsea inahitaji pointi sita tu kubeba taji kabla ya mechi hiyo ya usiku wa jana na hilo litakuwa taji lao la mbili ndani ya misimu mitatu na Matic kwa kutambua utamu wa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England aliamua kulibeba hilo kwa mikono yake kwa kumwahidi kocha wa West Ham United zawadi ya dina kwa kuichapa Spurs.

Bilic alisema Matic alimtumia meseji iliyosomeka hivi: "Kama utawazuia Tottenham, nitakupeleka dina." 

Manuel Lanzini akafunga bao pekee katika mechi hiyo kuimaliza Spurs na Bilic aliongeza: "Matic ni mtu safi sana na ni mchezaji mahiri. Nitaipokea ofa yake kwa furaha kubwa." 

Kocha wa Spurs, Mauricio Pochettino alisema kwamba licha ya kupoteza mechi hiyo, lakini wanachoamini ni kwamba mbio za ubingwa bado hazijafika tamati.

"Mambo bado," alisema Pochettino na kuongeza. "Tunasubiri, licha ya kwamba kuna ugumu wa kuikamata Chelsea. Inahuzunisha, tumepoteza nafasi muhimu ya kupunguza pengo la pointi."
Huu ndio ujumbe alioutuma Nemanja Matic kwa kocha wa West Ham Huu ndio ujumbe alioutuma Nemanja Matic kwa kocha wa West Ham Reviewed by Zero Degree on 5/09/2017 12:59:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.