Jinsi sakata la vyeti feki lilivyosababisha Zahanati 2 kubaki na mtumishi mmoja
Baada ya Rais John Magufuli hivi karibuni kutoa agizo kwa watumishi wa umma 9,932 waliobanika kuwa na vyeti vya kugushi, kuondoka kazini mara moja na kwamba watakaobakia kazini hadi Mei 15 wakamatwe ili sheria ichukue mkondo wake ikiwemo kufungwa jela miaka 7, na kuzitaka mamlaka zilizowaajiri kukata mishahara yao.
Agizo hilo limepelekea uhaba wa watumishi wa umma katika baadhi ya hospitali ambapo Mkoani Iringa kwenye hospitali ya Manispaa hiyo ya Frelimo imeondokewa na watumishi 10, wakati zahanati za Msisiwe na Ibumu zilizopo wilayani Kilolo zikibakiwa na mtumishi mmoja mmoja.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Iringa Dkt. William Mafwere, amesema kati ya watumishi 50 waliobainika kuwa na vyeti vya kugushi, 25 wanatoka idara ya afya huku akibainisha kwamba idara ya elimu mkoani hapo haijaathirika na zoezi hilo.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Iringa Dkt. William Mafwere, amesema kati ya watumishi 50 waliobainika kuwa na vyeti vya kugushi, 25 wanatoka idara ya afya huku akibainisha kwamba idara ya elimu mkoani hapo haijaathirika na zoezi hilo.
Jinsi sakata la vyeti feki lilivyosababisha Zahanati 2 kubaki na mtumishi mmoja
Reviewed by Zero Degree
on
5/08/2017 08:38:00 PM
Rating: