Loading...

Lipumba amekana kuhusika katika tukio la kupigwa kwa waandishi wa habari

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahimu Lipumba, amesema hahusiki na wala hakutoa maagizo kufanyike vurugu katika mkutano wa CUF wa wanachama wanaomuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharrif Hamad ambao waandishi wa habari walipigwa na kujeruhiwa na wavamizi.

“Nilisikitishwa sana na vurugu zilizotokea Dar es Salaam na waandishi wa habari kupigwa ieleweke kuwa sihusiki na wala sikutoa maagizo watu wapigwe,”alisema. 

Akizungumza leo wakati akihojiwa na kituo kimoja cha luninga jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja tu baada ya Maalim Seif kumshutum katika mambo kadhaa, Prof. Lipumba amesema kama Katibu Mkuu wa CUF angekuwa anaheshimu katiba ya chama kusingekuwa na matatizo kama yanayoendelea hivi sasa ndani ya chama.

“Tatizo ni kwamba chama chetu Katibu Mkuu wetu (Maalim Seif) anajiona sultani wa chama, anachotaka yeye ndiye kiwe, hataki kufuata Katiba na kimsingi yeye ndiye anaua chama,” amesema. 

Prof. Lipumba amesema yeye hatumiwi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kama ambavyo Maalim Seif amekuwa akidai na kwamba alianza kutofautiana na Katibu Mkuu wake tangu wakati wa mchakato wa Bunge la Katiba.

“Tulianza kusigana wakati wa mchakato wa Bunge la Katiba, kipindi hicho msimamo wa CUF ilikuwa ni kuwa na muungano wa serikali tatu lakini Maalim Seif akaja na msimamo wake wa kutaka kuwe na serikali ya muungano wa mkataba,”alisema.
Lipumba amekana kuhusika katika tukio la kupigwa kwa waandishi wa habari Lipumba amekana kuhusika katika tukio la kupigwa kwa waandishi wa habari Reviewed by Zero Degree on 5/04/2017 06:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.