Loading...

Mahakama ya kikatiba kutoa uamuzi juu ya sakata llinalomkabili Rais Zuma

Mahakama ya kikatiba nchini Afrika Kusini inatarajiwa kutoa uamuzi kama wabunge wanaweza kupiga kura ya siri ya kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma au la.

Hatua hiyo ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais huyo imesababishwa na Rais huyo aliyekuwa ziarani hapa nchini wiki iliyopita, kumfuta kazi waziri wa fedha na naibu wake miezi miwili iliyopita.

Mbali na hilo pia nchini humo kumekuwa na hali ya sintofahamu kuhusu uongozi wa Rais huyo huku kukiwa na madai ya ufisadi.

Upinzani unadai kwamba wabunge wanastahili kuongozwa na imani yao na sio uongozi wa vyama vyao kwa kuwa uongozi wa Rais Zuma ni suala muhimu kwa Taifa hilo.

Hata hivyo baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa wanaamini kwamba hata mahakama ya kikatiba ikiwapa wabunge haki ya kupiga kura kwa siri, wanachama wengi wa ANC watamuunga Rais Zuma.
Mahakama ya kikatiba kutoa uamuzi juu ya sakata llinalomkabili Rais Zuma Mahakama ya kikatiba kutoa uamuzi juu ya sakata llinalomkabili Rais Zuma Reviewed by Zero Degree on 5/15/2017 03:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.