Loading...

Mambo 5 muhimu yaliyojiri kwenye pambano la Antony Joshua na Wladimir Klitschko

ANTHONY Joshua na Wladimir Klitschko walionyesha uwezo wao kwenye pambano babu kubwa lililofanyika Jumamosi ya wiki iliyopita katika Uwanja wa Wembley.

Joshua alimwangusha Klitschko raundi ya tano kabla ya bondia huyo mwenye umri wa miaka 41 kumwonjesha mshindi wa medali ya dhahabu mwaka 2012, Joshua, jinsi wapinzani wanavyojisikia wakiangushwa baada ya kufanya hivyo raundi ya sita.

Ilionekana kama bingwa huyo wa zamani alitaka kumlazimisha refa kumaliza pambano hilo, lakini Joshua alipambana hadi kufanikiwa kumwangusha mkongwe huyo mara mbili kwenye raundi ya 11.

Joshua alifanikiwa kuendelea na rekodi yake ya kushinda mapambano 19 kati ya 19 yote kwa ‘knockout’ (KO), kujiwekea mazingira ya kuzipiga na bingwa wa WBC, Deontay Wilder ama Joseph Parker anayeshikilia mkanda wa WBO au Tyson Fury. Kuna mambo matano muhimu yaliyojiri kwenye pambano hilo.

Antony Joshua ni BINGWA kweli:

Akiwa ni bingwa wa Olimpiki na kufanikiwa kuchukua mkanda wa IBF katika mapambano yake 16, kuna watu walikuwa wakikosoa uwezo wa kupigana wa bondia huyo mwenye umri wa miaka 27.

Lakini sasa Joshua ameonyesha kumtwanga bondia yeyote wa uzito wa juu duniani, pia ameonyesha kwamba anaweza kushinda pambano gumu, baada ya kuanguka na kuamka na kumudu masumbwi makali aliyorushiwa na Klitschko na kuibuka na ushindi huo.

Akijua kwamba tayari Klitschko anatokwa damu, Joshua alirusha ngumi za kutosha akimwangusha Klitschko mara mbili kwenye raundi hiyo ya 11 na kushinda.

Klitschko naye ameonyesha kuwa ni bondia bora kweli:

Baada ya tukio la kushangaza la kupigwa na Tyson Fury, Novemba mwak 2015, wengi waliamini kwamba litakuwa pambano la upande mmoja kwa mkongwe huyo kupigwa raundi za mwanzo.

Ingawa amepigwa kwa ‘KO’, lakini pambano hili hakupigwa kama vile alivyodundwa na Lamon Brewster na Corrie Sanders.

Kwenye pambano hili dhidi ya Joshua alionekana kuwa mwepesi tofauti na alivyokuwa miaka saba iliyopita akiwa na kasi na umakini, akionyesha kwamba bado ni bondia wa kiwango bora.

Deontay Wilder:

Bondia wa Marekani, Deontay Wilder ‘Bronze bomber’, atataka kupigana na Joshua ambapo litakuwa pambano kubwa linalokutanisha wapinzani ambao wanaendana umri.

Hilo ndilo pambano pekee ambalo linakuja likimkutanisha Joshua na bondia huyo wa Marekani ambaye ana wastani wa asilimia 97 ya kutopigwa.

Katika mapambano yake 38 ameshinda 37 kwa ‘KO’ na bingwa huyo wa WBC alikuwamo katika Uwanja wa Wembley kama mchambuzi wa televisheni ya Sky Sports.

Joshua amewapiga Wamarekani watatu katika mapambano yake manne, lakini Wilder ataongeza utamu na kuwa bondia atakayempa upinzani Mwingereza huyo.

Nani zaidi?

Sasa Joshua na Tyson Fury wanakuwa mabondia waliompiga Klitschko hivi karibuni, lakini swali linakuja nani zaidi?

Bila shaka, bingwa mpya wa mkanda wa IBF, WBA na IBO alipata ushindi mtamu kuliko wa Fury.

Fury hakupewa nafasi ya kushiriki michezo ya Olimpiki mwaka 1996, lakini alimzidi Klitschko na kumshinda nchini Ujerumani.

Bondia huyo mzaliwa wa Jiji la Manchester, Fury, anatarajiwa kupewa leseni ya kupigana tena na akishajiweka sawa, staili yake ya kupigana itamsaidia kuonyesha uwezo wake kwa mara nyingine safari hii ikiwa kwenye Uwanja wa Wembley.

Joshua atafanya makubwa:

Joshua anaonekana kuwa bondia asiyepigika, ambapo anaweza akawa alishakuwa bingwa wa dunia kabla ya pambano la juzi Jumamosi usiku, lakini dhidi ya Klitschko lilikuwa pambano lake kubwa katika mapambano yake yote.

Si kwa kufanikiwa kuangushwa na kuamka na kushinda, lakini amekuwa kivutio anapofanyiwa mahojiano.

Hivyo kwa kushinda pambano hilo atakuwa ameshajitambua kwamba ni bondia bora, basi bila shaka ataendelea na kufanya makubwa zaidi mbeleni.
Mambo 5 muhimu yaliyojiri kwenye pambano la Antony Joshua na Wladimir Klitschko Mambo 5 muhimu yaliyojiri kwenye pambano la Antony Joshua na Wladimir Klitschko Reviewed by Zero Degree on 5/01/2017 08:44:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.