Loading...

Jacob Zuma azuiwa kutoa hotuba Siku ya wafanyazi nchini Afrika Kusini

Rais wa Afrika Kusini anayekumbwa na kashfa Jacob Zuma, ameondoka kwenye mkutano wa siku ya kimataifa ya wafanyazi baada ya kukemewa na wafanyakazi wanaomtaka ajiuzulu.

Fujo zilizuka kati ya wafuasi wa Bwana Zuma na wapinzani na kusabababisha hotuba yake kufutwa.

Chama kikuu cha wafanya kazi Cosatu, kilimtaka Bwana Zuma ajiuzulu mwezi uliopita baada ya kumfuta kazi waziri wa fedha alijekuwa akiheshimiwa sana.

Bwana Zuma ameapa kusalia ofisini hadi muhula wake ukamilike mwaka 2019.

Alionyeshwa na runinga akiondoka jukwaani kwa hasira na kuondolewa na magari kutoka kwa mkutano ulioandaliwa mjini Bloemfontein

Maafisa wa vyeo vya juu wa ANC nao walikemewa kwenye mkutano uliofanyika mjini Durban.

Shinikizo za kumtaka Zuma ajiuzulu zimekuwa zikoongezeka tangu amfute kazi waziri wa fedha Pravin Gordan mwezi Machi.

Kwa upande wake Rais Jacob Zuma, ameapa kusalia ofisini hadi muhula wake ukamilike mwaka 2019.
Jacob Zuma azuiwa kutoa hotuba Siku ya wafanyazi nchini Afrika Kusini Jacob Zuma azuiwa kutoa hotuba Siku ya wafanyazi nchini Afrika Kusini Reviewed by Zero Degree on 5/01/2017 08:29:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.