Loading...

Manchester United yaingia vitani dhidi ya Chelsea kusaka saini ya winga wa Fiorentina

Kwa mujibu wa Taarifa za mitandao , Mashetani wekundu sasa wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kusaka saini ya Winga wa Fiorentina, Federico Bernardeschi.

Raia huyo wa Italia amekuwa tamanio la vilabu vingi baada ya kuifungia Fiorentina magoli 14 katika mashindano yote msimu huu.

Chelsea nao pia wako kwenye mkakati wa kumsajili winga huyo wa Fiorentina kwa mujibu wa ripoti ya 'TransferMarketWeb'.

Yote haya yameibuka muda mfupi baada ya ripoti zilizodai Conte amemwambia mmoja wa wachezaji wake kuwa anaweza akaondoka kama hayuko tayari kujitoa kuitumikia klabu kwa moyo mmoja.

Hata hivyo, imeripotiwa pia kwamba, Bernardeschi yuko katika mazungumzo na Fiorentina kuhusu mkataba mpya.

Lakini, Ripoti nyingine inasema kwamba yuko katika mipango ya kuondoka Fiorentina.


Gazeti moja la Italia 'La Gazzetta dello Sport' lilisema mwezi mmoja tu umepita Meneja wa 'The Blues' alimshushia mezani kijana huyo mwenye miaka 23 dili la kuingiza pauni milioni 4.2 baada ya makato ya kodi kwa msimu.

Ofa hiyo inasemekana bado iko mezani pale Stamford Bridge na kwa kiasi cha fedha Chelsea imechokipata kutoka kuwa mshindi wa Ligi ya Uingereza ni dhahiri kwamba Conte anao uwezo wa kupambana.

Manchester United pia wanadaiwa kuwa kwenye mchakato wakuandaa ofa nzuri yakuweza kumnyakua winga huyo na wako tayari kuwapindua Chelsea, lakini ni habari ambazo hazijathibitiswa.

Barcelona, Bayern Munich, Inter Milan na Juventus nao pia inasemekana wanahitaji saini ya Bernardeschi.

Hata hivyo, inadaiwa aliwahi kuzungumzia kuhusiana na kuelekea klabu ya Juventus.

Pamoja na hayo yote, Bernardeschi bado ana mkataba na Fiorentina hadi mwaka 2019.
Manchester United yaingia vitani dhidi ya Chelsea kusaka saini ya winga wa Fiorentina Manchester United yaingia vitani dhidi ya Chelsea kusaka saini ya winga wa Fiorentina Reviewed by Zero Degree on 5/22/2017 02:04:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.