Loading...

Kauli ya Mourinho baada ya Manchester United kuchapwa goli 1-0


Jose Mourinho amesifia kiwango kilichoonyeshwa na Newcastle United katika mchezo wa timu hiyo dhidi ya Manchester United uliomalizika kwa mashetani wekundu kupigwa goli 1-0.

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho ameeleza kuwa kitendo cha timu yake kufungwa goli 1-0 na Newcastle United siku ya Jumapili ni “kizuri”.

Mashateni wekundu wamepoteza mechi ya pili mfululizo wakiwa ugenini katika Ligi Kuu ya Uingereza. Shukruni kwa goli pekee na la ushindi lililofungwa na Matt Ritchie mnamo dakika ya 65, ambalo liliongeza idadi ya michezo ambayo ilimalizika kwa Jose Mourinho kutoka na matokeo mabovu katika dimba la St James.

Kwa upande wake Mreno huyo alionekana kufurahia matokeo yale na badala ya kuwalaumu wachezaji wake kwa kuonyesha kiwango kibovu aliimwagia sifa Newcatle kwa kupata ushindi.

“Walipigana kama wanyama na wanastahili pongezi. Walijitoa kwa kila kitu na miungu soka ilikuwa pamoja nao. Haikua kwa ajili yetu lakini pia hata wao walijitoa kwa vyote na hicho ni kitu kizuri sana katika mpira wa miguu. Lazima watakuwa na furaha sana kwa sasa,” alisema Mourinho na kuongeza:

“Nafikiri la msingi ni walilokuwa nalo akilini mwao. Tulifanya makosa katika safu ya ulinzi wakati mpira wa adhabu ulipopigwa na walipokuwa mbele walijitoa kwa kila kitu kuhakikisha wanapata matokeo mazuri. Hawakua pekee yao, miungu ya soka  pia ilikuwa pamoja nao, lakini ilikuwa ni walitumia njia nzuri kupata ushindi.”
Kauli ya Mourinho baada ya Manchester United kuchapwa goli 1-0 Kauli ya Mourinho baada ya  Manchester United kuchapwa goli 1-0 Reviewed by Zero Degree on 2/11/2018 11:56:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.