Loading...

Matokeo ya uchaguzi EALA kwa wagombea wa Chadema

Bunge la Tanzani jana limepiga kura na kuwachagua wabunge wawili wa CHADEMA watakaoungana na wenzao 7 kutoka CUF na CCM kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

Uchaguzi huo wa wabunge wa CHADEMA ulirudiwa jana baada ya wagombea wa kwanza kukataliwa bungeni kwa kupigiwa kura ya hapana kwa kile kilichoelezwa kuwa hawakuwa wamekidhi vigezo.

Katika uchaguzi wa jana, wabunge wawili waliochaguliwa ni Josephine Sebastian Lemoyan na Pamela Pamela Maasay.

Katika kinyang’anyiro hicho wagombea wengine walikuwa nia Ezekiel Wenje, Lawrence Masha, Salum Mwalimu na Prof. Safari.

Matokeo ya uchaguzi kwa wagombea nafasi za ubunge wa Afrika Mashariki EALA kutoka Chadema.
  1. Profesa Abdalla Safarikura 35.
  2. Wenje kura 34
  3. Lawrence Masha kura 44
  4. Salim Mwalimu kura 54
  5. Josephine Lemoyan kura 219
  6. Pamela Maasay kura 200.
Washindi waliochaguliwa na wabunge.
  1. Josephine Lemoyan
  2. Pamela Maasay

Wabunge: 9
Wanaume: 4
Wanawake 5

Pamela Maasay
Josephine Lemoyan

Matokeo ya uchaguzi EALA kwa wagombea wa Chadema Matokeo ya uchaguzi EALA kwa wagombea wa Chadema Reviewed by Zero Degree on 5/11/2017 11:10:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.