Mexime yupo tayari kutua Yanga endapo uongozi utaridhia mapendekezo haya
Mexime amefanikiwa kutwaa tuzo ya kocha bora wa msimu akiwa na kikosi chake cha Kagera Sugar, alichokiongoza kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo.
Hivi karibuni kuna taarifa ambazo DIMBA ilizibaini kuwa Yanga ipo kwenye mawindo mazito ya kumvuta kocha huyo viunga hivyo, kuchukua nafasi ya Juma Mwambusi, anayetarajiwa kutupiwa virago.
Akizungumza jana, Mexime alisema bado hajapata taarifa rasmi kutoka ndani ya uongozi wa Yanga, lakini amekiri kuwa, kama Yanga watakuabaliana na matakwa yake, kwa maana ya dau analotaka pamoja na vigezo vingine, hatakuwa na tatizo la kutua ndani ya kikosi hicho.
Alisema hawezi kuweka ni kiasi gani anakitaka kwa kuwa bado hawajafanya mazungumzo yoyote mpaka sasa, lakini pia amesisitiza anahitaji ushirikiano miongoni mwa wachezaji na viongozi pamoja na pamoja na nidhamu ambayo kwa upande wake ameitaka kama ndio siri yake ya mafanikio.
Naye Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, alisema taarifa za Mexime kutua Yanga hawezi kuzizungumzia kwa sasa, kwa kuwa bado hana taarifa za kina juu ya ujio wake ndani ya timu hiyo.
Mexime ameifundisha Kagera Sugar kwa mafanikio makubwa na kujikuta ikimaliza ligi kuu ikiwa nafasi ta tatu na kabla ya hapo aliifundisha Mtibwa Sugar na iliweza kufanya vizuri.

“Mkataba wangu na Kagera Sugar unamalizika mwezi wa saba na sasa tupo kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba mwingine, habari za Yanga kunihitaji nimekuwa nikizisikia tu.
“Siwezi kuweka wazi sana, lakini kikubwa kama wataridhia matakwa yangu sina tatizo lolote kwa sababu kazi yangu haichagui timu, kikubwa ni maelewano, ukiachilia suala la maslahi, vipo vitu vingine lazima vizingatiwe, likiwepo suala zima la nidhamu kwa wachezaji,” alisisitiza Mexime.
Naye Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, alisema taarifa za Mexime kutua Yanga hawezi kuzizungumzia kwa sasa, kwa kuwa bado hana taarifa za kina juu ya ujio wake ndani ya timu hiyo.
Mexime ameifundisha Kagera Sugar kwa mafanikio makubwa na kujikuta ikimaliza ligi kuu ikiwa nafasi ta tatu na kabla ya hapo aliifundisha Mtibwa Sugar na iliweza kufanya vizuri.
Mexime yupo tayari kutua Yanga endapo uongozi utaridhia mapendekezo haya
Reviewed by Zero Degree
on
5/28/2017 07:06:00 PM
Rating: