Loading...

Mkurugenzi wa Shirika la ujasusi la FBI atumbuliwa

Rais wa Marekani Donald Trump, amemtumbua mkurugenzi wa shirika la ujasusi la FBI kutokana na hatua yake ya kuchunguza suala la barua pepe za aliyekuwa mgombea wa uraisi wa chama cha Democrat Hillary Clinton, mamlaka imesema.

Ikulu ya Whitehouse iliishangaza Washington kwa kutangaza kwamba James Comey ametimuliwa.

Lakini wanachama wa Democrats wamesema kuwa alifutwa kazi kwa sababu FBI ilikuwa ikuchunguza madai ya uhusiano kati ya Trump na Urusi.

Hatua hiyo inajiri baada ya kubainika kwamba bwana Comey alitoa habari za uongo kuhusu barua pepe za Clinton kwa bunge la Congress wiki iliopita.

Rais Trump aliandika barua kwa bwana Comey kwamba alikubaliana na mapendekezo ya mwanasheria mkuu Jeff Sessions kwamba ameshindwa kuliongoza vizuri shirika hilo.

Bwana Sessions alisema kuwa idara ya haki ina nidhamu ya hali ya juu, uadilifu na sheria na mwanzo mpya unahitajika.

Ikulu ya Whitehouse imesema kuwa utafutaji wa mrithi wake unaanza mara moja
Mkurugenzi wa Shirika la ujasusi la FBI atumbuliwa Mkurugenzi wa Shirika la ujasusi la FBI atumbuliwa Reviewed by Zero Degree on 5/10/2017 09:23:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.