Loading...

Mpanda milima maarufu duniani, Ueli Steck afariki dunia wakati akijaribu kupanda mlima Everest

Mmoja wa wapanda milima maarufu zaidi duniani Ueli Steck, amefariki katika Mlima wa Everest.

Steck ambaye alikuwa akiitwa Mashine ya Uswiswi, alifariki kwenye ajali, alipokuwa akijaribu kufanya mazoiezi ya kupanda mlima huo kwa kupitia njia mpya bila ya kutumia gesi ya oxygen.

Steck, alikuwa na umri wa miaka 40, na ameshinda tuzo kadha huku akijulikana kwa kukwea milima kwa kasi.

Mwili wake umetolewa mlima Everest na kupelekwa mji mkuu wa Nepal, Kathmandu.

Ueli Steck aliweka reko mpya wa kukwea milima kwa kasi na kutumia njia mpya.

Pia alichangia katika mchezo huo kupata mashabiki wapya kutokana na filamu kumhusu zilizotengezwa.

Mwaka 2015 alipanda moja ya kuta maarufu zaidi duniani unaofahamika kama North Face of the Eige, kwa muda wa saa 2 na dakika 47, jaribio lililowachukua watangulizi wake siku kadha kukamilisha.

Ueli Steck amewahi kufanikiwa kupanda mlima Everest awali bila hewa ya oxygen
Mpanda milima maarufu duniani, Ueli Steck afariki dunia wakati akijaribu kupanda mlima Everest Mpanda milima maarufu duniani, Ueli Steck afariki dunia wakati akijaribu kupanda mlima Everest Reviewed by Zero Degree on 5/01/2017 12:49:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.