Mwanajeshi apigwa picha wakati wa kifo chake katika ajali ya mlipuko Afghanistan
Mwanajeshi Hilda Clayton mwenye umri wa miaka 22 na wanajeshi wanne wa Afghanistan waliuawa wakati bomu lilipolipuka wakati wa zoezi la kijeshi mnamo tarehe 2 mwezi Juali 2013.
Jeshi la Marekani pia lilitoa picha ya mwanajeshi wa kike wa Afghanistan ambaye mtaalam Clayton alikuwa akijifunza naye kupiga picha ambaye pia alifariki.
Kifo cha Clayton ni ishara kwamba wanajeshi wa kike wanazidi kukabiliwa na hatari wakati wa mafunzo pamoja na vita na wenzake wa kiume.
Ajali hiyo ilitokea katika mkoa wa mashariki wa Laghman.
Jarida la jeshi lilichapisha picha hizo.
Picha hii ilichukuliwa na mwanajeshi mwengine ambaye alikuwa akijifunza na Clayton |
Clayton [miaka 22]alikuwa mkaazi wa jimbo la Georgia nchini Marekani |
Mwanajeshi apigwa picha wakati wa kifo chake katika ajali ya mlipuko Afghanistan
Reviewed by Zero Degree
on
5/04/2017 09:47:00 AM
Rating: