Loading...

Nahodha wa Simba, Jonas Mkude anusurika kwenye ajali ya gari iliyoua moja wakati wakirejea Dar


Kiungo na nahodha wa timu ya Simba SC, Jonas Mkude amepata ajali baada ya gari alilokuwa akisafiria na abiria wengine kupinduka katika eneo la Dumila mkoani Morogoro wakati wakirejea jijini Dar es salaam kutokea Dodoma.

Gari lenye namba za usajili T 834 BLZ, Toyota VX alilokuwa akisafiria nahodha wa timu ya Simba, Jonas Mkude, na wenzake ambao hawakufahamika mara moja, likiwa limepinduka na kuanguka vichakani katika barabara ya Dodoma-Dar es Salaam.
Ajali hiyo iliyohusisha gari yenye namba za usajili T 834 BLZ, Toyota VX imetokea baada ya gurudumu la nyuma ya gari hiyo kupasuka na kusababisha majeruhi wawili ambapo wamewahishwa kwenye hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Shabiki mmoja amefariki dunia katika ajali hiyo iliyotokea katika eneo la Dumila mkoani Morogoro.

Kiungo na nahodha wa timu ya Simba SC, Jonas Mkude
Mkude ni kati ya majeruhi na wengine watatu pia wameumia na tayari wako njiani wakitoka Dumila kupelekwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Muslah Al Rawah amethibitishwa kwa majeruhi hao kupelekwa Morogoro.

Mkude alikuwa njiani kutoka Dodoma kurejea Dar es Salaam baada ya jana Simba kuitwanga Mbao FC kwa mabao 2-1 na kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho.


Nahodha wa Simba, Jonas Mkude anusurika kwenye ajali ya gari iliyoua moja wakati wakirejea Dar Nahodha wa Simba, Jonas Mkude anusurika kwenye ajali ya gari iliyoua moja wakati wakirejea Dar Reviewed by Zero Degree on 5/28/2017 04:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.