Loading...

Willian amefunguka kuhusiana na 'Future' yake Chelsea

Willian ameonekana mwenye dalili za kutaka kuendelea kubakia na klabu yake ya Chelsea kwa msimu ujao, hali iliyopo inaonyesha kabisa kwamba hataondoka 'The Blues'.

Kumekuwepo na mambo mengi yaliyokuwa yakisemwa Kuhusiana na maisha yajayo ya soka ya Wilian ambapo uvumi huo ulianza kuzagaa kufuatia kukosa muda wa kutosha wa kucheza uwanjani akiwa na Meneja wake mpya, Antonio Conte.

Hata hivyo, Mbrazili huyo amesema kwamba, suala la yeye kuondoka Chelsea ni kitu kisichowezekana kwani anajiandaa na Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) akiwa na 'The Blues' msimu ujao wa 2017/18
.

Willian aliueleza mtandao wa Chelsea kabla ya Fainali ya FA Cup: “Ninafuraha kwa sababu kila wakati nilipopata nafasi ya kucheza niliifungia goli au kuisaidia timu yangu kushinda kwa namna moja au nyingine.


“Cha msingi ninafuraha kwa sababu tumemaliza msimu kama Mabingwa. Kiukweli nilikuwa na wakati mgumu sana mwanzoni mwa msimu, ambo nahisi kila mmoja analifahamu hilo, lakini baada ya pale nilijitoa kwa nguvu kwa ajili ya timu.”

Aliongeza: “Mwezi Agosti nitakuwa nimetimiza miaka minne hapa, nimekwisha shinda kombe la Ligi Kuu mara mbili na kombe la Ligi moja."
Willian amefunguka kuhusiana na 'Future' yake Chelsea Willian amefunguka kuhusiana na 'Future' yake Chelsea Reviewed by Zero Degree on 5/28/2017 04:34:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.