Loading...

Conte atishia kumuuza Willian endapo hatotimiza hili

Kulingana na Ripoti za mitandao, Meneja wa Chelsea, Antonio Conte inadaiwa amemuonya Willian kuwa atamuuza endapo hatojitoa kwa moyo mmoja kwa Klabu yake.

Ikumbukwe kwamba, Willian amekua akihusishwa na Uhamisho kwenda klabu ya Manchester United, ambao wanaonekana wanahitaji huduma yake na kiongozi wa mkakati huo akiwa ni Jose Mourinho.

Willian amekuwa akipigania kupata nafasi uwanjani pale Stamford Bridge kwa msimu huu ambapo Chelsea imenyakua Ubingwa wa Ligi Kuu.


Ripoti zinadai kwamba Conte bado anahitaji kuwa na Willian kikosini, Hata hivyo, yuko tayari pia kumuuza kama atataka kuondoka.
Wakati muitaliano huyo alipoulizwa kuhusu Willian, alisema: "Kwanza ya yote mchezaji lazima awe na furaha kuwa Chelsea (Kwa ujumla awe na mapenzi ya kweli na klabu).


“Hili ni jambo la kwanza muhimu sana. Kwangu mimi ni muhimu sana.

“Kila mchezaji anayetaka kubaki na klabu lazima awe na furaha kwa kubakia klabuni.”


Conte pia hivi karibuni amekiri kwamba Mancester United wanamuhitaji Willian.

Alieza hivi: “Manchester United wameonekana kumuhitaji, ni kweli, na ni kwa sababu Mourinho naye yuko pale ambaye pia anamwelewa Willian.”
Conte atishia kumuuza Willian endapo hatotimiza hili Conte atishia kumuuza Willian endapo hatotimiza hili Reviewed by Zero Degree on 5/21/2017 02:46:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.