Loading...

Nay afunguka kuhusiana na mafanikio ya 'WAPO'

RAPA Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ anayesumbua na Wimbo uitwao Wapo, hivi karibuni amefunguka namna wimbo huo ulivyomletea mafanikio ndani ya muda mfupi tangu auachie jambo ambalo kwake ni kama maajabu.

Nay alizidi kufunguka kuwa miongoni mwa mafanikio ambayo wimbo huo uliompa misukosuko umempatia ni kubadilishwa lugha na ‘media’ mbalimbali za nje zikiwemo BBC na CNN ili dunia nzima iweze kuupata ujumbe alioulenga lakini pia shoo ambazo hazikatiki.

“Tofauti na nyimbo zangu zote, Wapo umenipa mafanikio sana. Naona ni kama maajabu maana kila wiki napiga shoo kuanzia tatu lakini pia umenifanya kuwa karibu na viongozi wa kiserikali na ambao hawapo serikalini. Lakini pia ni kujulikana zaidi nje ya nchi maana media za nje zimenizungumzia sana,” alimalizia.
Nay afunguka kuhusiana na mafanikio ya 'WAPO' Nay afunguka kuhusiana na mafanikio ya 'WAPO' Reviewed by Zero Degree on 5/01/2017 12:47:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.