Loading...

Vodacom kukabidhi vifaa ligi kuu

Meneja Uhusiano wa Vodacom wanaodhamini ligi hiyo, Matina Nkurlu.

TIMU zitakazoshiriki ligi kuu ya msimu ujao zitakabidhiwa vifaa mbalimbali kwa ajili ya ligi hiyokwenye hafla itakayofanyika Alhamisi jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana, Meneja Uhusiano wa Vodacom wanaodhamini ligi hiyo, Matina Nkurlu alisema kuwa vifaa hivyo jezi, viatu na nguo maalum za mazoezi vitatolewa ikiwa ni ishara ya kuelekea kwenye msimu mpya wa ligi kuu.

“Vifaa vyote kwa ajili ya ligi ya msimu ujao vipo tayari kilichobakia ni kuvikabidhi siku ya alhamisi ili timu ziweze kuendelea na maandalizi,” alisema Nkurlu.

Alisema hafla ya kukabidhi vifaa hivyo itaudhuriwa pia na viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), viongozi wa klabu pamoja na baadhi ya wachezaji.

Ligi kuu imepangwa kuanza Agosti 20 mwaka huu na tayari TFF imeshatoa ratiba ya mzunguko wa kwanza.

ZeroDegree.
Vodacom kukabidhi vifaa ligi kuu Vodacom kukabidhi vifaa ligi kuu Reviewed by Zero Degree on 8/02/2016 10:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.