Loading...

Picha: Polisi yaua majambazi wanne Kariakoo, jijini Dar

Jeshi la Polisi limewaua watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakati wakivamia maduka Kariakoo, Mtaa wa Aggrey / Livingstone usiku wa kuamkia leo.



Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa majibizano ya risasi kati ya polisi na majambazi yalichukua takribani dakika 10 huku majambazi hao wakionekana kuzidiwa na kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi hao.

Imeelezwa kuwa, kutokana na purukushani hizo za majibizano ya risasi kati ya majambazi na jeshi la polisi, baadhi ya watu waliokuwa eneo la tukio wamejeruhiwa kwa risasi ambapo mmoja wao amepelekwa hospitali.






<<<<<<Endelea kufuatilia Ukurasa huu kwa Taarifa zaidi>>>>>>
Picha: Polisi yaua majambazi wanne Kariakoo, jijini Dar Picha: Polisi yaua majambazi wanne Kariakoo, jijini Dar Reviewed by Zero Degree on 5/20/2017 04:29:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.