Loading...

Polisi wazingira mgodi baada ya RC kuzuiliwa kuingia ndani


Jeshi la Polisi limeuzingira mgodi wa Bulyanhulu baada ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellaack kuzuiwa kuingia katika mgodi huo alikokwenda kukagua iwapo uzalishaji unaendelea bila kuwepo kwa Maofisa wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini (TMAA).


Jeshi hilo limefanya hivyo baada ya Tellack kuagiza kuimarisha ulinzi katika eneo lote la mgodi huo kuhakikisha hakuna mtu anyetoka wala kuingia.

Ilivyokua Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kuzuiwa kuingia mgodi wa Bulyamhulu:

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellack 
Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellack umezuiwa kuingia katika mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu alikokwenda kukagua iwapo uzalishaji unaendelea bila kuwepo kwa Maofisa wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini(TMAA).

Maofisa hao waliondoka mara baada ya ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa dhahabu kupokelewa na Rais John Magufuli.

Tellack anayefanya ziara ya kikazi wilayani Kahama amesema ameagiza jeshi la polisi kuimarisha ulinzi katika eneo lote la mgodi huo kuhakikisha hakuna mtu anyetoka wala kuingia.

Mapema leo, mkuu huyo wa mkoa alitembelea mgodi mwingine wa Buzwagi ambao pia unamilikiwa na kampuni ya Acacia kama ulivyo ule wa Bulyanhulu.

Katika mgodi wa Buzwagi, Tellack na msafara wake waliruhusiwa kuingia na kishuhudia shughuli za uchimbaji ukiwa umeshitishwa kwa kukosekana maofisa wa TMAA walioondoka mara baada ya Rais Magufuli kutangaza kuvunja bodi na kutengua uteuzi wa watendaji wakuu wa wakala hiyo.
Polisi wazingira mgodi baada ya RC kuzuiliwa kuingia ndani Polisi wazingira mgodi baada ya RC kuzuiliwa kuingia ndani Reviewed by Zero Degree on 5/25/2017 07:21:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.