Loading...

Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Tamisemi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 24 Mei, 2017 amemteua Tixon Tuliangine Nzunda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) - anayeshughulikia Elimu.

Kabla ya uteuzi huo, Tixon Tuliangine Nzunda alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.

Bw. Tixon Tuliangine Nzunda anachukuwa nafasi ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) - akishughulikia Elimu Bw. Bernard Makali ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.

Uteuzi huu unaanza mara moja.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
24 Mei, 2017
Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Tamisemi Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Tamisemi Reviewed by Zero Degree on 5/24/2017 09:54:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.