Loading...

Taarifa ya Kamati Maalum ya kuchunguza mchanga wa madini yatinga kwa Rais Magufuli

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, inawataarifu wananchi wote kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 24 Mei, 2017 atapokea Taarifa ya Kamati Maalum aliyoiunda kuchunguza mchanga ulio katika makontena ya mchanga wa madini (Makinikia) yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini Tanzania.

Tukio la kupokea taarifa hiyo litahudhuriwa na viongozi mbalimbali na kurushwa moja kwa moja kupitia vituo vya habari vya redio, televisheni na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz

Wananchi mnakaribishwa kutazama na kusikiliza matangazo hayo yatakayorushwa hewani kuanzia saa 3.30 Asubuhi kutoka Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Taarifa ya Kamati Maalum ya kuchunguza mchanga wa madini yatinga kwa Rais Magufuli Taarifa ya Kamati Maalum ya kuchunguza mchanga wa madini yatinga kwa Rais Magufuli Reviewed by Zero Degree on 5/24/2017 10:01:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.