Loading...

Sababu za Nahodha wa Serengeti Boys, Issa Makamba kurudishwa Tanzania

May 20, 2017, Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania TFF Alfred Lucas akiwa Gabon alizungumza kuhusiana na nahodha wa timu ya taifa ya vijana ya Serengeti Boys, Issa Abdi Makamba kurudishwa Tanzania.


Makamba akiwa mazoezini aliumia siku tatu kabla ya kuanza kwa mashindano ya AFCON U-17, hivyo jina lake likaondolewa katika orodha ya Wachezaji wa Serengeti Boys watakaoshiriki michuano hiyo japokua aliendelea kubaki kambini na timu.

Taarifa za uhakika ni kwamba leo (20 May, 2017) amerudishwa Tanzania licha ya kuwa awali viongozi walisema atakuwa na wenzake hadi mwisho wa mashindano, ni nini kilichofanya arudishwe Tanzania? 

Majibu ya swali hilo yalitolewa na afisa habari wa TFF, Alfred Lucas kama ifuatavyo:


“Ni kweli amerejea nyumbani na kilichofanya arudishwe ni sababu kuu mbili za Madaktari watatu, CAF walileta mchezo mmoja Port Gentil na yeye kwa hali yake haipaswa asafiri hivyo inakua kama kumsumbua zaidi” 

"Sababu nyingine ni kwamba anapoendelea kubaki na Wachezaji wenzake na kuhudhuria mechi akiwa benchi inazidi kumuumiza zaidi sababu anatamani angekua anacheza, Madaktari wameshauri arudishwe tu Tanzania"
Sababu za Nahodha wa Serengeti Boys, Issa Makamba kurudishwa Tanzania Sababu za Nahodha wa Serengeti Boys, Issa Makamba kurudishwa Tanzania Reviewed by Zero Degree on 5/21/2017 12:09:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.