Loading...

Tumbaku marufuku kusafirishwa toka wilaya mmoja hadi nyingine mkoani Tabora

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri amepiga marufuku usafirishaji wa tumbaku kutoka wilaya moja kwenda nyingine ili kudhibiti utoroshaji unaotarajiwa kufanya nabaadhi ya wakulima wasio waaminifu ambao hadi hivi sasa wamekaidi agizo la Waziri Mkuu la kuwataka wakulima wote kuuza tumbaku yao kupitia Vyama vya Msingi vilivyopokatika maeneo yao.

Marufuku hiyo inafuatia wakulima wa kujitegemea (IF) zaidi ya 16 kutoka Wilaya ya Urambo na Uyui kukataa kujisajili katika Vyama vya Msingi na hivyo kutoonyesha kuwa watauzia tumbaku yao kupitia Chama gani cha Msingi.

Mkuu wa Mkoa huyo alitoa agizohilo jana mjini Tabora wakati wa kikao cha wadau wa tumbaku, Kamati ya Ulinzina Usalama ya Mkoa , ambapo pamoja na mambo mengine kupitia Bodi ya TumbakuTanzania kimejadili tarehe ya kuanza kwa  masoko ya tumbaku ambayo yataanza siku ya Ijumaa wiki hii katika meneo mbalimbali.

Alisema kuwa Serikali iliamuawakulima wote kuuzia tumbaku yao kupitia Vyama vya Msingi katika maeneo yao nasio vinginevyo ili kuepuka watu wanatumia mwanya wa kujitegemea kuwarubuni tumbaku ya wakulima wadogo wadogo walipokatika vyama vya msingi na kuwauzia baadhi ya tumbaku yao na kusababisha madenikatika vyama vyao vya Msingi.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa hadi hivi sasa baadhi ya wakulima hao wamekata kujisajili katika Vyama vya Msingi vilivyopo katika maeneo yao na hata kwingine ni ishara tosha kuwa wanampango wakutorosha tumbaku hiyo kwenda kuuzia wanakujua kinyume na agizo la Waziri Mkuu.

Alisisitiza kuwa yeye akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa, hawezi kukubali watuwakaidi agizo la Waziri Mkuu kwa nia ya kutaka kuwanyonya wakulima wengine.

Kufuatia hali hiyo aliagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Wilaya kushirikiana na Watendaji ngazi za chinina kuwakamata wao na mizigo yote itakayokuwa inasafirisha nje ya eneo la Chama cha Msingi la Mkulima anapokaa kama bidhaa hiyo haijanunuliwa na kupata hati inayotambulika na Bodi ya Tumbaku ya Tanzania (TTB) na wanunuzi rasmi watumbaku wenye vibali vya kufanya kazi hiyo mkoani Tabora.Atoa angalizo kwa vyombo vyote vinavyotumika kusafirisha tumbaku kutoka eneo moja kwenda jingine kuhakikisha mzigo waliopakia katika magari unavibali vyote baada ya ununuzi katika soko kupitia Chama cha Msingi ili kuepuka usumbufu na kuchukuliwa hatua.

Katika hatua nyingine Mkuu huyowa Mkoa ameagiza Wakurugenzi Watendaji, Maafisa Ushirika, Wanasheria na Wawakilishiwa Benki za CRDB na NMB kukaa meza moja na kuangalia uwezekano wa kuwekamakubaliano ambayo yatawahakikisha wakulima wote wa tumbaku ambao walilima kwakutumia pembejeo zao wasiathirike na makato ya madeni ya wakulima wanaodaiwa.

Alipendekeza kuwepo na Akauntimbili, moja ni ile inayomlinda mkulima wa aliyejitegemea na nyingine yawakulima ambao wanadaiwa ili kila mtu apate haki kulingana na alivyojiandaakatika kilimo hicho.

Mkuu huyo wa Mkoa alisisitizakuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha kuwa hakuna atakayenyimwa haki yake kwasababu ya watu wengine.

Hata hivyo wadau hao wa tumbakuwalisema hakuna  haja ya kuwa na akauntimbili badala yake Benki zinaweza kuweka utaratibu mzuri wa utambuzi wa mtualiyelima kwa kujitegemea na kumpa fedha zake zote na wale wanaodaiwawakaendelea na utaratibu wanaoutumia.

Walisema kuwa hatua itawasaidia wakulima waliojitegemea na kuamua kuuzia tumbaku yao kupitia vyama vya msingikupata haki yao bila kuchelewa kwa kusubiri deni la Chama cha Msingi limalizike kwanza ndio walipwe.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Tabora, Dkt. Thea Ntara amesema kuwa baadhi ya matatizo na migogoro katika zao latumbaku yamesababishwa na maslahi binafsi ya baadhi ya watumishi wakiwemo Maafisa Ugani, Maafisa Ushirika, Wafanyakazi wa Mabenki na watumishi wengine wanaojihusisha ununuzi usio halali wa zao hilo na kilimo hicho.

Alisema kuwa watumishi hao ndio wamekuwa wakichochea migogoro na wengine kuwarubuni wakulima kwa kununua tumbaku yao kinyume cha utaratibu na kuwafanya walaze madeni.

Dkt. Ntara alisema kuwa ili zaohilo limsaidie mkulima ni vema wataalumu wakafanyakazi zao za utaalam kuliko kuwa washindani wa wakulima na hivyo wakati kuanzisha migogoro kwa maslahi yao binafsi ili hatimaye wakulima wakate tamaa na kuanza kuuza tumbaku katika masoko yasiyo rasmi.
Tumbaku marufuku kusafirishwa toka wilaya mmoja hadi nyingine mkoani Tabora Tumbaku marufuku kusafirishwa toka wilaya mmoja hadi nyingine mkoani Tabora Reviewed by Zero Degree on 5/23/2017 10:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.