Loading...

Umeisikia hii ya Bia inayotengenezwa kwa kutumia mkojo?

Kiwanda kimoja cha pombe nchini Denmak kimetengeneza bia mpya ambapo ngano huchanganywa na lita 50,000 za mkojo.


Hata hivyo bia hiyo haitakuwa na mkojo wa binadamu.

Mkojo huo ulikusanywa kutoka kwa hafla moja kubwa zaidi ya muziki barani ulaya miaka miwili iliyopita.

"Wakati habari kuwa tulikuwa tumeanza kutengeneza pombe zilifichuka, watu walidhani kuwa tilikuwa tukiweka mkojo huo moja kwa moja kuenda kwa pombe," alisema mkurugenzi wa kampuni ya Norrebro Bryghus.

"Kama ingekuwa na ladha ya mkojo ningeachana nayo, lakini hata huwezi ukahisi," alisema mtu moja ambaye alihudhuria warsha hiyo ya muziki mwaka 2015.

Lita hizo 50,000 zilizokusanywa kutoka kwa warsha hiyo ya muziki zilitosha kuunda chupa 60,000 za bia.

Mashini iliyotengenezwa na kundi la wanasayansi katika chuo kimoja nchini Ubelgiji, inabadili mkojo wa binadamu na kuwa maji ya kunywa pamoja mbolea ikitumia nguvu za miale ya jua.
Umeisikia hii ya Bia inayotengenezwa kwa kutumia mkojo? Umeisikia hii ya Bia inayotengenezwa kwa kutumia mkojo? Reviewed by Zero Degree on 5/09/2017 10:00:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.