Loading...

Upelelezi wa kesi ya madawa ya kulevya inayomkabili Masogange wakamilika

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imeambiwa kwamba upelelezi wa kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili msanii Agnes Gerald Waya, maarufu kama Deal ama Masogange (28), umekamilika na itaanza kusikilizwa maelezo ya awali Juni 13.

Masogange jana alifika mahakamani kusikiliza kesi yake na kudai kuwa siku iliyotolewa hati ya kukamatwa wakati ilipotajwa Machi 21, alichelewa kwa bahati mbaya.

Kesi hiyo ilitajwa jana mbele ya Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri.

Hakimu alimhoji mshtakiwa kwa sababu gani tarehe iliyopita hakuhudhuria mahakamani, akajibu kwamba alifika lakini alichelewa na kukuta ameshatoa amri ya kukamatwa.

Hakimu Mashauri alisema kesi hiyo itasikilizwa maelezo ya awali Juni 13.

Awali kabla ya kupangwa tarehe ya kusikilizwa, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na aliomba mahakama kupanga tarehe ya kusikiliza.

Katika kesi ya msingi, Masogange anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin na oxazepam.

Aidha mpamba video za muziki huyo anadaiwa kufanya makosa hayo chini ya kifungu cha 18 (a) cha Sharia ya Kupambana na dawa za kulevya namba 5 ya mwaka 2015.

Katika kesi hiyo namba 77 ya mwaka 2017, Masogange anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14, mwaka huu katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).

Aidha, anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14 hiyo alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.

Masogange yupo nje kwa dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao kila mmoja alisaini bondi ya Sh. milioni 10 na kutotoka nje ya jiji la Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha mahakama.
Upelelezi wa kesi ya madawa ya kulevya inayomkabili Masogange wakamilika Upelelezi wa kesi ya madawa ya kulevya inayomkabili Masogange wakamilika Reviewed by Zero Degree on 5/10/2017 10:13:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.