Loading...

VIDEO: Pamoja na kichapo cha goli 2-1 jana, Real Madrid imetinga fainali ya UEFA

Real Madridi wametinga fainali ya UEFA kwa jumla ya magoli 4 kwa 2, ikiwa ni idadi ya magoli yote yaliyopatikana katika michezo yote miwili. Jana walikubali kichapo cha goli 2-1 toka kwa mahasimu wao Atletico Madrid. Mchezo wa jana ulikuwa wa pili katika nusu fainali hiyo, baada ya mchezo mwingine uliopigwa Santiago Bernabeu kumalizika kwa Real Madrid kuibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Atletico.

Magoli ya Atletico jana yalifungwa na Niguezi katika dakika ya 12 na la pili likifungwa na Antonie Griezmann kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 16. Goli la Real Madrid lilifungwa na Isco katika dakika ya 42.

Kwa matokeo hayo, Real Madrid inawafuata Juventus kwenye Fainali ya Ligi ya Mabingwa ulaya (UEFA), ambao walitangulia awali kwa kuwatoa Monaco.

VIDEO: Pamoja na kichapo cha goli 2-1 jana, Real Madrid imetinga fainali ya UEFA VIDEO: Pamoja na kichapo cha goli 2-1 jana, Real Madrid imetinga fainali ya UEFA Reviewed by Zero Degree on 5/11/2017 09:41:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.