Loading...

Walionusurika kwenye ajali ya basi la Lucky Vincent kufadhiliwa masomo hadi Chuo Kikuu

Baraka zimeendelea kumiminika kwa watoto watatu, majeruhi wa ajali ya basi la shule ya Lucky Vincent, baada ya Shirika la Elimu la Marekani kuwapa ufadhili wa masomo watoto hao kwa kuwasomesha bure hadi Chuo Kikuu.

Watoto watakaopata ufadhili huo ni Saidia Ismail, Wilson Tarimo na Doreen Mshana.

Bodi ya wadhamini ya Shirika hilo la elimu kati ya Tanzania na Siouxland, Marekani, (Stemm) limetoa ufadhili huo kama sehemu ya kuwaenzi wanafunzi 32 waliopoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea Karatu, Mei 6 mwaka huu.

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ameandika katika ukurasa wake wa facebook na ksuema kuwa Stemm,imeamua kuwapa ufadhili huo ili kuhakikisha maisha ya watoto waliofariki katika ajali hiyo na watatu kati yao kupona yanabaki katika kumbukumbu daima
Walionusurika kwenye ajali ya basi la Lucky Vincent kufadhiliwa masomo hadi Chuo Kikuu Walionusurika kwenye ajali ya basi la Lucky Vincent kufadhiliwa masomo hadi Chuo Kikuu Reviewed by Zero Degree on 5/23/2017 05:36:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.