Wanafunzi walionusurika kwenye ajali ya basi Arusha wapelekwa Marekani leo
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akiwaaga majeruhi hao Uwanja wa Ndege wa KIA kabla ya kusafirishwa. |
Ndege hiyo ya Samaritan’s Purse DC 8 N782SP imewasili Kilimanjaro Tanzania jana Mei 13, 2017 ikiwa na marubani wanne na wahudumu saba tayari kuwabeba majeruhi hao ambao wataambatana na wazazi wao mpaka Marekani kwa matibabu.
Rubani wa ndege hiyo, amewaambia waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) kwamba baada ya kuondoka, watasimama Cape Verde kuweka mafuta kisha kuelekea Marekani moja kwa moja na wanatarajia kuingia kesho.
Ndege hii imetolewa na shirika la SAMARITAN’S PURSE linalosimamiwa na mtoto wa mwinjilisti mkubwa wa Marekani, Franklin Graham, familia yao baada ya kupelekewa habari za kilichotokea kwenye ajali ya Karatu walikubali kuituma ndege hiyo kutoka Marekani kuja kuwachukua majeruhi Tanzania.
Ndege hiyo imeondoka Mei 14, majira ya mchana ikiwa imewabeba watoto hao watatu na mama zao, nesi mmoja na daktari mmoja wa Kitanzania ambao wataendelea kuwahudumia watoto hao ndani ya ndege hiyo yenye uwezo wa kutoa huduma kama ambulance pia.
Ndege hiyo ikishatua North Carolina, SAMARITAN’S PURSE wameandaa ndege nyingine ambayo pia inaweza kufanya kazi kama AMBULANCE na kuwachukua hadi Jimbo la Iowa ambako Hospitali ya Mercy imekubali kuwatibu wagonjwa hao bure kwa muda wote watakaohitaji matibabu.

Wazazi wa watoto hao watatu wakionyesha hati za kusafiria za kuingia Marekani pamoja na watoto wao na wako tayari kwa safari. |
Vitanda vya ndani ya ndege |
Wanafunzi walionusurika kwenye ajali ya basi Arusha wapelekwa Marekani leo
Reviewed by Zero Degree
on
5/14/2017 11:56:00 PM
Rating: