Zahanati 2 zafungwa mkoani Songwe baada ya kukumbwa na sakata la vyeti feki
Mkuu wa mkoa wa Songwe, Chiku Galawa |
Mkuu wa mkoa wa Songwe Chiku Galawa mbele ya wakuu wa idara na watumishi,amesema watumishi 98 wamebainika kuwa na vyeti vya kugushi na kwamba sekta ya afya imeathirika zaidi ambapo zahanati mbili alizozitaja kuwa ni Songambele iliyopo wilaya ya Songwe na ifuko iliyopo walayani Momba zimefungwa kufuatia watoa huduma za afya 57 kukumbwa na sakata vyeti vya kugushi.
Baadhi ya watumishi wa serikali waliosalimika wamesema kutokana na mkoa wa Songwe kuwa mpya umekuwa na changamoto ya upungufu mkubwa wa watumishi kabla ya sakata hilo,na kwamba sasa changamoto imeongezeka maradufu kiasi kwamba kazi za watu kumi sasahivi zinafanywa na mtu mmoja, hivyo wameiomba serikali kuu kuharakiasha taratibu za ajira ili kuziba mapengo yaliyojitokeza.
Kutokana na upungufu huo, Mkuu wa mkoa Mh. Galawa ametaja mkakati uliopo katika kujaza nafasi zilizoachwa wazi kuwa Ofisi ya Rais Utumishi imetangaza nafasi za kazi elfu kumi na tano na kuwataka watumishi kujipanga na kujituma kuhakikisha huduma zinaendelea kutolewa wakati wakisubiri serikali kuongeza watumishi wengine.
Aidha, wananchi wamebariki zoezi la kubaini watumishi wenye vyeti vya kugushi na kusema kuwa sio kazi nyepesi kwa kuwa inagusa watu wengi ambao hawawezi kulifurahia jambo hilo hivyo kuitaka serikali ikaze buti kuendeleza mapambano.
Zahanati 2 zafungwa mkoani Songwe baada ya kukumbwa na sakata la vyeti feki
Reviewed by Zero Degree
on
5/21/2017 06:23:00 PM
Rating: