Loading...

Baada ya Mdee na Bulaya, Spika amewaonya wabunge wengine watatu

Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai
WAKATI Halima Mdee na Ester Bulaya wakizuiwa kuonekana bungeni hadi mwakani, Spika Job Ndugai ametoa onyo kwa wabunge wengine watatu wa upinzani kutokana na kutoa maneno machafu dhidi yake na chombo hicho cha kutunga sheria.

Jana Bunge liliazimia kuwafungia kuhudhuria mikutano yake mitatu kuanzia wa Bunge la Bajeti unaoendelea mjini hapa wabunge hao wa Kawe na Bunda Mjini (Chadema) kutokana na kufanya vurugu na kudharau mamlaka ya Kiti wakati Spika Ndugai alipoagiza askari wamtoe bungeni Ijumaa iliyopita Mbunge wa Kibamba, John Mnyika (Chadema).

Baada ya adhabu hiyo kutolewa dhidi ya wawili hao jana, Spika Ndugai alitoa onyo kwa wabunge wengine wanne kutoka vyama vinavyunga Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) akidai Ijumaa walitoa maneno machafu dhidi yake na Bunge yakiwamo ya kumtukana.

Mbali na Chadema, vyama vingine vinavyounda Ukawa ni CUF, NLD na NCCR-Mageuzi) lakini NLD hakikupata uwakilishi bungeni katika uchaguzi mkuu uliopita.

Spika Ndugai alisema kuwa baada ya wabunge wa upinzani kutoka kwenye Ukumbi wa Bunge Ijumaa iliyopita wakipinga kutolewa nje kwa Mnyika, baadhi yao walitamka maneno machafu dhidi yake na wabunge waliobaki ndani, yaani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Maftaha Nachuma, Mbunge wa Mtwara Mjini -CUF) ambaye hakutoka ukumbini kuungana na wabunge wengine wa Ukawa.

Aliwataja wabunge hao ambao alidai walinaswa na mitambo ya Bunge wakiporomosha maneno dhidi yake na Bunge kuwa ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi, Rhoda Kunchela (Chadema) na Mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga (Chadema) na Mbunge wa Tandahimba, Ahamed Katani (CUF).
Baada ya Mdee na Bulaya, Spika amewaonya wabunge wengine watatu Baada ya Mdee na Bulaya, Spika amewaonya wabunge wengine watatu Reviewed by Zero Degree on 6/06/2017 10:41:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.