Kamati ya Uongozi ACT kukutana July 7, kujadili hatima ya nafasi ya Mghwira
Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma Ado Shaibu iliyotolewa leo, inaeleza kuwa Mama Mghwira ambaye wakati wa uteuzi wake alikuwa nje ya nchi, baada ya kurejea amefanya mazungumzo na viongozi wa juu wa chama hicho kuhusu uteuzi wake.
Aidha, chama hicho kimetoa wito kwa wanachama wake kuendelea kuwa watulivu wakati wa vikao vya chama vinachukua hatua stahiki kuhusu jambo hili.
“Kufuatia uteuzi huo na kwa kuzingatia unyeti na majukumu ya mkuu wa mkoa kamati ya uongozi ya chama itakutana kesho juni 7 kutafakari pamoja na mambo mengine namna ambavyo mama mghwira atatekeleza wajibu wake wa uenyekiti wa chama na majukumu yake mapya,” inaeleza taarifa hiyo.
Aidha, chama hicho kimetoa wito kwa wanachama wake kuendelea kuwa watulivu wakati wa vikao vya chama vinachukua hatua stahiki kuhusu jambo hili.
Kamati ya Uongozi ACT kukutana July 7, kujadili hatima ya nafasi ya Mghwira
Reviewed by Zero Degree
on
6/06/2017 10:36:00 AM
Rating: